Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi awaita Wananchi kwa Mkapa "Sitawangusha "

Yanga Mashabiki Ks Gamondi awaita Wananchi kwa Mkapa "Sitawangusha "

Fri, 24 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Young Africans SC, Miguel Gamondi amewaita mashabiki kujitokeza uwanjani kwa wingi kushuhudia burudani pindi timu hiyo itakapoikabili Tabora United, kesho Jumamosi.

Young Africans SC kesho Jumamosi watakuwa wenyeji wa Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Katika mchezo huo ndio watakabidhiwa ubingwa wa Ligi Kuu walioshinda msimu huu kwa msimu wa tatu mfululizo na mara ya 30 kwa ujumla.

“Nafahamu mashabiki wetu kesho wanatamani kupata burudani ya kutosha. Nina matumaini makubwa sana kuwa watapata burudani. Sitawangusha kwani kila mara wamekuwa wakitoa mchango wao mkubwa kwetu. Njooni kwa Mkapa wananchi mtafurahi,” alisema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live