Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi awaita Wananchi kwa Mkapa

Gamondiz1462 Gamondi awaita Wananchi kwa Mkapa

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Young Africans SC, Miguel Gamondi, amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanjani Jumamosi katika mchezo dhidi ya CR Belouizdad.

Jumamosi ya wiki hii, timu ya Young Africans SC itapambana na CR Belouizdad katika mchezo wa Kundi D wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kuelekea mchezo huo, Gamondi alisema: “Jumamosi ni mchezo wa lazima kushinda, tunataka kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, tunataka kushindana, tunafahamu tupo katika moja ya kundi gumu.

“Wananchi ni sehemu ya mafanikio kwetu, jinsi wanavyotusapoti, unakumbuka mechi dhidi ya Medeama.

“Hata dhidi ya Al Ahly, tuliruhusu goli lakini mashabiki wakaendelea kutusapoti, hii kwangu ni tukio bora zaidi katika maisha yangu kuona mashabiki kama hawa Wananchi.

“Ninaamini Jumamosi watakuja na kuujaza uwanja, Wananchi tutawapa kila kinachowezekana, tutapigana kwa ajili ya jezi hii, siwezi kuahidi ushindi moja kwa moja, lakini tutapambana kushinda, ninaamini tutacheza vizuri, wawe pamoja nasi, itakuwa vizuri sana kuona uwanja ukijaa.”

Mchezo huo ni muhimu kwa Yanga kushinda kwani tutajitengenezea nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo.

Hivi sasa katika msimamo wa Kundi D, Young Africans ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi tano sawa na CR Belouizdad, tofauti ni magoli ya kufunga na kufungwa, Al Ahly wanaongoza wakiwa na pointi sita, wakati Medeama wanazo nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: