Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi awaandalia Singida FG kosi la maangamizi

Gamondi Gift 3 WA0008 Gamondi awaandalia Singida FG kosi la maangamizi

Sat, 13 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wa kesho Jumapili dhidi ya Singida Fountain Gate, Kocha Mkuu wa Young Africans SC, Miguel Gamondi amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya kuendelea kufanya vizuri.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC, unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kuanzia saa 10 jioni.

Gamondi amesema: “Leo jioni tutafanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Singida na mazoezi yetu ya leo yatatupa mwelekeo wa wachezaji gani tutaweza kuwatumia kwenye mchezo wa kesho.

“Maandalizi ni ya kawaida kwa sababu tumetoka kucheza juzi na tunajua mchezo wa kesho utakuwa mgumu, lakini tumejiandaa kuhakikisha tunafanya vizuri.

“Falsafa ya kwanza ya Young Africans SC ni timu na siyo mchezaji mmoja mmoja, wenyewe mmekuwa mashahidi michezo yetu iliyopita tulikuwa na majeruhi, lakini kila mchezaji aliyepata nafasi ya kucheza amefanya kazi yake vizuri.

“Napenda pia kuwapongeza Mashabiki wetu kwa kazi nzuri wanayoifanya kila mahali tunapokwenda kucheza na nilishangaa mashabiki wetu wa Mwanza kwenye mchezo tuliocheza hapa dhidi ya Geita, walikuwa wanashangilia kwa nguvu muda wote wa mchezo, ilikuwa ni kama niko Amerika Kusini, najua kesho watakuja kwa wingi kutupa sapoti.”

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji, Gift Fred amesema: “Kwa niaba ya wachezaji wenzangu tumejiandaa vizuri na mchezo wa kesho, kwetu sote kila mchezo ni muhimu na kila mmoja wetu anayepata nafasi kuwa katika kikosi cha kwanza atahakikisha anajituma ili tupate ushindi.”

Mpaka sasa, Young Africans SC inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa kukusanya pointi 52 baada ya kucheza mechi 20.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live