Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi avunja rekodi ya Nabi

Nabi Gamondi Pc Gamondi avunja rekodi ya Nabi

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga chini Masta Miguel Gamondi imekuwa na ubora mkubwa hasa katika utengenezaji wa nafasi pamoja na matumizi ya nafasi hizo,kumbuka huu ndio msimu wa kwanza tu wa Gamondi.

Kwanini nasema Yanga imevunja rekodi ya Yanga? Msimu uliopita wa 2022/23 chini ya Kocha Nasreddine Nabi katika mechi 18 Yanga ilikuwa imefunga magoli 36 na kufungwa goli 10.

Msimu huu wa 2023/24 hadi inacheza mechi ya 18 jana dhidi ya Ihefu,takwimu zinaonyesha kuwa Yanga imefunga goli 47 ikiwa ongezeko za goli 11.

Yanga mpaka sasa imefungwa mabao 9 ikiwa ndiyo timu pekee iliyofungwa mabao machache kwenye Ligi Kuu ya NBC.

Nini maana yake? Ni kwamba ubunifu katika eneo la mwisho la Yanga umeongezeka.

Nani atamzuia Yanga kubeba Ubingwa msimu huu?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live