Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi atua na faili zito Yanga, wachezaji wakuna vichwa

Gamondiss Miguel Gamondi

Sat, 8 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga wamempokea Kocha wao Mkuu Miguel Gamondi jana Ijumaa amewasili nchini kuja kuanza kazi rasmi, lakini usije kushtuka ni kwamba jamaa anashuka na faili moja zito ambalo linaweza kuwakata baadhi ya mastaa wa kikosi hicho kama tulivyowadokeza mapema.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba kocha Gamondi atatua nchini kuja kukutana uso kwa uso na mabosi wa Yanga ikiwa ni mara ya kwanza tangu apewe kibarua cha kuwafundisha mabingwa hao wa soka nchini akichukua nafasi ya Mtunisia Nasreddine Nabi.

Ujio wa Gamondi unaweza kuwa na presha kubwa kwa baadhi ya mastaa walioitumikia timu hiyo msimu uliopita ambapo ameachiwa nafasi ya kuja kumalizia usajili kwa kuwapitisha waliosalia na kama atahitaji mtu mpya.

Inafahamika dhahiri kwamba, tayari Gamondi ameshawapa uwazi mabosi wa Yanga kwamba kwa mifumo yake anahitaji watu wanaoshambulia na kujua kutengeneza nafasi za mabao na kufunga na kwamba usajili wao ujikite hapo.

"Kuna watu ambao tunaweza kuja kuwapa mkono wa kwaheri tumemuachia yeye kocha aje afanye maamuzi hayo kwa jicho lake, wale ambao alituhimiza tuwabakishe tumefanya hivyo na wengine tunaendelea kuzungumza nao zaidi," alisema bosi wa juu wa Yanga.

Inaelezwa Gamondi akishamalizana na mabosi wa Yanga atakutana na wachezaji wote wakiwamo waliosalia nchini na wale walioenda na Malawi kwa ajili ya mchezo maalum wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa juzi mjini Lilongwe dhidi ya Big Bullets katika maadhimishi ya huru wa nchi hiyo.

Mastaa kutambulishwa kishua

Mashabiki wa Yanga jana kila mtu presha juu wakipambana kupata uzi wao mpya wa msimu huu ambao mabosi wao waliutambulisha kisasa kule Malawi huku wakiweka rekodi ya kuzinduliwa na marais wa nchi mbili za Malawi na Tanzania.

Katika uzinduzi huo uliofanyika Ikulu ya Malawi, Yanga ilitumia nafasi ya kukutana kwa marais Lazarus Chakwera na Samia Suluhu Hassan wa Tanzania ambao ndio waliozindua jezi hizo za msimu ujao.

Kikosi hicho kitararejea jana alfajiri nchini tayari kwa kuaanza maandalizi ya mwisho ya kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya itakayoanza Julai 10 hapa nchini.

Wakati marais hao wakizindua jezi hizo, Yanga itatumia pia utambulisho wa wachezaji wao wapya kutangazwa na uzi huo mpya wakianza na kocha wao Gamondi ambaye aliyetambulishwa leo alfajiri.

Nyota wengine wapya waliosajiliwa na ambao wapo kwenye orodha ya kutambulishwa hivi karibuni, kila mmoja atambulishwa kishua na uzi huo tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita wachezaji walivishwa na kutambulishwa na jezi za nyuma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: