Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi atoa msimamo CAFCL

Gamondi 547 Kocha Gamondi

Sun, 8 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ametoa msimamo wake kwa kusema hataki kurudia makosa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, akipania kuinoa safu ya ushambuliaji kutumia kila nafasi watakazopata ili kufika mbali zaidi, huku akisistiza kwamba hakuna aliyejihakikishia namba eneo hilo.

Gamondi amefunguka hayo muda mfupi baada ya kushuhudia timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ikiambulia suluhu dhidi ya Ethiopia kwenye Uwanja wake Benjamin Mkapa.

Akizungumza na Mwanaspoti, alisema licha ya Yanga kutajwa kuwa bora kila eneo, lakini kwa upande wake anaumizwa kichwa na mastaa wa timu hiyo katika suala la upachikaji wa mabao kitu ambacho anapambana nacho kabla ya  mchezo wa Septemba 14 dhidi ya CBE ya Ethiopia.

“Hatua hii ni muhimu na itategemea matokeo mazuri nyumbani na ugenini tunaanzia ugenini tunahitaji ushindi wa mabao mengi ili kukwepa kuondolewa kwa changamoto ya idadi ya mabao ya nyumbani na ugenini kama hatua ya robo fainali msimu uliopita,”  alisema Gamondi.

“Kila mchezo ni muhimu kwetu tumeanza vizuri katika hatua ya awali kwa kushinda mechi zote mbili kwa idadi nzuri ya mabao. Natarajia hilo litaendelea hatua ijayo na kwenye hili sina mchezaji ambaye namtegemea eneo hilo, kila mchezaji wajibu wake ni kuipambania timu.”

Gamondi alisema hana wasiwasi na ushindani atakaokutana nao kwani anauelewa ugumu wa michuano hiyo na wachezaji wake wanatambua umuhimu wa mchezo na malengo ya msimu huu.

“Tutaingia kwa kuwaheshimu wapinzani wetu tumeshasahau matokeo yaliyopita mipango ya mchezo ujao inaendelea vizuri na mipango ni kufanya vizuri ugenini ili kuja kumaliza mchezo kwenye uwanja wetu wa nyumbani,” alisema.

Kocha huyo alisema kwa ujumla timu hiyo mbali na mastaa walio katika vikosi vya timu za taifa, waliopo wanaendekea na maandalizi kwa kujiandaa na mechi za CAF sambamba na zile za Ligi Kuu Bara.

Mwanaspoti linafahamu kwenye kikosi cha Ethiopia kuna wachezaji wanne wa CBE ambayo itakutana na Yanga hatua ya pili Ligi ya Mabingwa, na alipoulizwa Gamondi kama alienda Kwa Mkapa kuwaangalia mastaa hao ambao watatu kati yao walianza kikosi cha kwanza, alisema hapana.

“Mimi ni kocha na napenda mpira nilikuja uwanjani kutazama mpira na kuwapa sapoti Taifa Stars,”  alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live