Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi atoa kauli kwa Coastal Union

Gamondi Coastal Kocha Gamondi.

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa kikosi cha Yanga SC, Miguel Gamondi, amezungumzia mchezo wa kesho Jumatano wa Ligi Kuu ya NBC tutakaocheza dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mchezo huo wa raundi ya tisa ambao tutacheza ugenini, tutaingia uwanjani tukiwa vinara katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC tukiwa na pointi 21.

“Kwa kweli, siwezi kusema mengi kuhusu maandalizi kwa sababu, kama unavyojua, tulikuwa na shughuli nyingi za maandalizi wiki iliyopita kwa ajili ya mchezo wa dabi.

"Tulicheza Jumapili na jana tulifanya mazoezi ya kurejesha utimamu wa mwili ili kuona hali ya wachezaji tunaosafiri nao. Leo tutafanya mazoezi madogo pamoja na mambo mengine na benchi la ufundi.

“Tunaendelea kufanya uchambuzi wa video ya mechi dhidi ya Coastal Union na leo tutachunguza zaidi, kwa hivyo maandalizi kwa ajili ya mchezo huu ni hayo tu.

“Kawaida, michezo kama hii huathiri upande wa kimwili na ufitnesi wa wachezaji. Baada ya mchezo mgumu kama wa Jumapili iliyopita, wachezaji wanaweza kupata majeraha madogo na ukijumlisha safari ndefu ya masaa sita kwa basi baada ya mchezo, kupona huwa ngumu kidogo. Jambo jema ni kwamba tulipata matokeo mazuri sana ambayo yanatuhamasisha, kila mtu amejituma.

“Kwa kweli, sitazami sana nafasi ya timu tunayocheza nayo kwa sababu mara nyingine matokeo huwa ni bahati. Ninawaheshimu, nimeshuhudia baadhi ya michezo ya Coastal Union, mara nyingine wamepoteza michezo vibaya na mara nyingine kwa bahati mbaya, lakini soka ni hivyo, kila mchezo ni tofauti. Naamini kwamba timu zilizo katika nafasi kama hii, wanapocheza dhidi ya timu kubwa kama Yanga inayoshika nafasi za juu, zitapambana na kuwa na hamasa.

“Natarajia mchezo mgumu kwetu. Uwanja si rafiki kwa aina yetu ya mchezo. Lakini tunahitaji kucheza na kuona nini kitatokea. Lakini tunawaheshimu wapinzani,” alisema Gamondi.

Kuhusu kupumzisha wachezaji?

“Mtaweza kuona kesho, labda kutakuwa na wachezaji ambao hawawezi kucheza kwa sababu ya matatizo. Tunao wachezaji wawili au watatu wenye majeraha kidogo. Sijui kama watapona kwa Jumatano, lakini kwa uwezekano wao watapona,” alibainisha Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live