Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi ataka mechi moja

Pacome Gamondi Maxi Gamondi ataka mechi moja

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema anahitaji mechi ya kirafiki kabla ya kukutana na wapinzani wao CR Belouidad ya Algeria kwenye mechi ya kwanza ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Gamondi amesema hayo baada ya kukaa na mastaa wake kwa muda wakifanya mazoezi ya kujiweka fiti na kuwaangalia wapinzani nao namna kikosi chao kilivyo ikiwemo mbinu zao.

Yanga itacheza mchezo huo Novemba 24, mwaka huu ikianzia ugenini katika Uwanja wa Julai 5, 1962, Algeria, kuanzia saa 4.00 usiku.

“Tumepata mapumziko kutokana na ligi kusimama kwa mechi za timu za mataifa mbalimbali, tunafanya sana mazoezi kuhakikisha tunakuwa bora katika mchezo ujao, tunahitaji mchezo wa kujipima.

“Nimezungumza na viongozi watafute timu ambayo utatupa ushindani tucheze nao Jumamosi hii, baada ya mchezo huo ndio tutafanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo mkubwa,” amesema Gamondi

Kocha huyo amesema ameanza kuwafuatilia wapinzani wao kuona wanacheza michezo ya aina gani, kuhakikisha anapata mbinu za kukabiliana nao.

Gamondi amesema anatambua kuwa wapinzani wao wana kikosi bora na ushindani mkubwa, anakiandaa kikosi chake kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mchezo wa kwanza.

Amesema kazi kubwa ni kufanya tathimini ya wapinzani ambao wanakutana nao anataka kujua ubora na udhaifu wao hasa wanapokuwa nyumbani.

Katika mashindano hayo, Yanga imepangwa kundi D na timu za CR Belouizdad, Medeama ya Ghana na Al Ahly ya Misri.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: