Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi ataka mabao zaidi Yanga

Miguel Gamondi Caf Press Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki wa Yanga wanaendelea kuchekelea baada ya kushuhudia timu hiyo ikianza Ligi Kuu kwa kishindo ikiifumua KMC mabao 5-0, akizungumzia soka hilo Kocha Gamondi licha ya kuwapongeza wachezaji wake lakini ametoa kauli akionyesha kuhitaji mabao zaidi kutokana na wingi wa nafasi wanazozitengeneza.

“Vijana walicheza kwa ubora mkubwa kuanzia nyuma na eneo la kiungo tulionekana kutulia na kuwabana vizuri wapinzani wetu, tunawaheshimu sana wapinzani wetu ni timu nzuri lakini nadhani tulistahili ushindi mkubwa zaidi ya huu,”

“Tunatengeneza nafasi nyingi za kufunga kwa mfano mzuri kipindi cha kwanza ambacho hatukutulia kutumia nafasi nyingi tutaendelea kuhimizana kuongeza umakini, jambo zuri tunaona viungo, washambuliaji na hata mabeki wanafunga hii itawoangezea hali ya kujiamini kwenye mechi zijazo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: