Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi ataka kumchapa konde mwamuzi - Video

Gamondi A68Q.jpeg Gamondi ataka kumchapa konde mwamuzi - Video

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amezua taharuki baada ya kutaka kumchapa makonde mwamuzi msaidizi (line 2) wa mechi dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa jana katika Dimba la Azam Complex, Chamazi.

Tukio hilo lilitokea baada ya kumalizika kwa mchezo huo huku chacho kikitajwa kuwa ni mwamuzi huyo kukataa bao alilofunga mshambuliaji wa Yanga, Joseph Guede akionesha kuwa alikuwa kwenye eneo la kuotea kabla ya kufunga.

Katika marejeo ya picha, yalionesha Guede hakuwa eneo la kuotea hivyo lilikuwa bao halali licha ya mwamuzi huyo kukataa bao hilo.

Baada ya mchezo kumalizika, Gaomondi alimfata mwamuzi huyo kwa gadhabu akitaka kumchapa huku Aziz Ki na Skudu wakimshikilia na kumsihi asifanye kitendo hicho, na baadaye kocha huyo alitulizwa na kutoka ndani ya uwanja huku akifoka.

Kutokana na tukio hilo, huenda Gamondi akakumbana na adhabu ya TFF kwa kosa kumfanyia fujo mwamuzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live