Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi ataja sababu ya kutoanza na Konkoni

Gamondi X Konkoni Gamondi ataja sababu ya kutoanza na Konkoni

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Klabu ya Young Africans, Miguel Gamondi ametaja sababu za kutomwanzisha kwenye mechi zake mshambuliaji wake mpya Hafiz Konkoni akisema kuwa bado anampika zaidi.

Gamondi amesema kuwa Konkoni ni mshambuliaji tegemeo hivyo lazima amlinde kwa kumuandaa vizuri kisaikolojia, kumuondolea presha kwa kumpa dakika chache kisha baadae akiiva ataanza kumtumia kama atakavyo.

"Ninampa muda mchache Mshambuliaji Hafiz Konkoni kwa sababu ya kumlinda.Mchezaji tegemeo anapaswa kuanza taratibu kama ilivyokuwa kwa Aziz Ki pamoja na Pacome Zouzoua ili kumtolea pressure ya mashabiki na wachambuzi mpaka atakapokuwa fit zaidi.

"Mashabiki na wachambuzi wanaweza ondoa ufanisi wa mchezaji. Taratibu ataingia kikosini na ataanza kucheza kwa dakika nyingi hivi karibuni," amesema Kocha Miguel Gamondi.

Itakumbukwa kuwa Konkoni ambaye amesajiliwa kutoka Ghana alicheza mchezo wa (1) wa mashindano kwa dakika 8, akaja kucheza mchezo wa pili dakika 10 na dhidi ya KMC alicheza dakika 28 na kufunga bao moja na assist moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: