Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi ashusha beki mwingine wa kati Yanga

Shaibu Mtita Shaibu Mtita

Sun, 10 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga ikionekana kuwa na utajiri wa mabeki wa kati, kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi ameongeza beki mwingine kwenye eneo hilo anayekwenda kuwania namba na kina Dickson Job na nahodha Bakari Mwamnyeto.

Yanga ina mabeki wanne wa kati Job, Mwamnyeto, Ibrahim Abdallah ‘Bacca’ na Gift Fred na sasa Gamondi amemuongeza ‘bwana mdogo’ Shaibu Mtita akimpandisha kutoka kwenye timu ya vijana.

Shaibu yupo Yanga kwa muda mrefu katika timu za vijana, lakini baada ya Gamondi kumuona moja kwa moja akamwambia kocha wa timu ya vijana ya U-20, Saidi Maulid (SMG), kumwambia kinda huyo ajiunge na timu kubwa tayari kwa kambi ya kuanza msimu huu.

“Hata mimi nilishtuka kwani nilipigiwa simu na kocha wangu wa U-20, SMG, na kuambiwa kocha Gamondi ananitaka mazoezini kwa wakubwa na baada ya hapo kila kitu kilienda vyema na sasa nipo hapa na timu kubwa,” alisema Shaibu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: