Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi apiga 'hat-trick'

Gamondi Yanga Mussa Kocha Gamondi

Sun, 5 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi, amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa Mwezi Aprili 2024 katika Ligi Kuu ya NBC ikiwa ni kwa mara ya tatu msimu huu.

Tuzo hizo tatu alizoshinda Gamondi mpaka sasa unaweza kusema amepiga hat trick kutokana na kuibuka kidedea Agosti 2023, Februari 2024 na Aprili 2024.

Gamondi ameshinda Tuzo ya Mwezi Aprili baada ya kuwashinda Bruno Ferry (Azam) na Malale Hamsini (JKT Tanzania).

Ndani ya mwezi Aprili 2024, Gamondi ameiongoza Yanga kucheza mechi nne, akishinda tatu na sare moja, huku pointi kumi zikikusanywa.

Katika mechi hizo nne, matokeo yalikuwa hivi; Singida Fountain Gate 0-3 Yanga, Yanga 2-1 Simba, Yanga 1-0 Coastal Union na JKT Tanzania 0-0 Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live