Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi anazitaka alama tatu za Simba SC

Gamondi Press Miguel Gamondi

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi raia wa Argentina, amefichua kwamba, ana kazi kubwa mbele ya kuhakikisha anapata matokeo mazuri katika michezo yake mitatu ijayo ikiwemo dhidi ya Simba SC kabla ya kugeukia michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa lengo la kupunguza presha ya kupambania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Gamondi ametoa kauli ikiwa Young Africans ina michezo mitatu dhidi ya Singida Fountain Gate (Oktoba 26), Simba (Novemba 5) na Coastal Union (Novemba 8), kisha watageukia Ligi ya Mabingwa Afrika kupambana na CR Belouizdad ya Algeria kati ya Novemba 24 na 25.

Kabla ya mchezo wa jana Jumatatu 9Oktoba 23) dhidi ya Azam FC iliyokubali kupigwa 3-2, Young Africans ilikuwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na alama 12 na sasa ipo kileleni kwa kufikisha alama 15 sawa na Simba SC, wakati Azam FC ikiporomoka hadi nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 13.

Gamondi amesema moja ya jukumu kubwa ambalo lipo mbele yake ni kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo hiyo kwa kuwa wanataka kupunguza presha kubwa iliyopo kwao baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Ihefu katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Tumepoteza mchezo ambao hatukutarajia, kwa sasa tunajaribu kuweka malengo katika michezo ambayo ipo mbele yetu kwa sababu ya kupunguza pengo la pointi na kubaki kwenye kile ambacho tunatarajia kukifanya msimu huu.

“Ukweli ni kwamba, ligi ni ngumu, lakini hatuwezi kusema tunataka kurudi nyuma kwa sababu hizi mechi ambazo zipo mbele yetu zinahitaji kupata matokeo mazuri kabla ya kuanza kuangalia michuano ya kimataifa.

“Nataka kuona timu inashinda hizi mechi kabla ya kuangalia Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu dhamira ya kutetea ubingwa wetu msimu huu haiwezi kupotea,’ amesema Gamondi

Chanzo: Dar24
Related Articles: