Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi anapita njia ya Nabi - Jemedari Said

Nabi Gamondi 2 WA0002 Nabi na Gamondi

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia EFM,Jemedari Said Bin Kazumari amesema kuwa anachokifanya Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi ni kilekile alichokuwa akikifanya mtangulizi wake, Nasreddine Nabi wakati akikinoa kikosi hicho.

Jemedari amesema hayo kufuatia matokeo mazuri inayoyapata Yanga chini ya Gamondi sambamba na kutumia mfumo na falsafa ileile aliokuwa akiutumia Nabi ya kumiliki zaidi mpira, kushambuli, kujilinda kwa nidhamu na hata kufanya rotation ya wachezaji wake ili kuwapa nafasi wachezaji wote kuonyesha uwezo wao.

"Moja kati ya kazi ngumu kwa kocha ni kuusoma mchezo na kufanya mabadiliko ya mchezaji ambaye analeta manufaa uwanjani.

"Nikukumbushe, msimu uliopita kwenye Ngao ya Jamii, kwenye ile mechi ya Simba dhidi ya Yanga, kipindi cha kwanza kinaisha kwa Simba kuongoza 1-0, na kipindi cha pili Nassredine Nabi anafanya mabadiliko kwa kumuingiza Bernard Morrison na Jesus Moloko kisha wanaingia na kufanya mabadiliko yaliyotoa nafasi kwa Yanga kufanya vizuri na kushinda mechi 2-1, magoli yote yakifungwa na Fiston Mayele.

"Mabadiliko kama yale yamekuwa yakifanywa sana tu na Nabi na hapo alidhihirisha ubora wake sababu hiyo ni kazi ngumu sana kwa kocha.

"Hicho ndicho anakifanya Gamondi kwa sasa, na mfano mfupi ni mchezo huo wa juzi nchini Rwanda, mabadiliko aliyoyafanya yameleta faida kubwa na tukubaliane Gamondi anapitia kwenye msingi mzuri uliojengwa na Nabi," amesema Jemedari Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: