Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi amwachia msala Eng. Hersi

Miguel Gamondi Akubali.jpeg Kocha Gamondi

Sat, 27 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi kukabithi ripoti kwa uongozi wa klabu hiyo kuhitaji kusajiliwa wachezaji watano katika msimu ujao na baadhi ya Wachezaji wanaomaliza mikataba yao waongezewe mikataba na mpaka sasa uongozi wa klabu ya Yanga ya imeanza mazungumzo na wachezaji waliopendekezwa na kocha huyo.

Wachezaji ambao wamependekezwa na Muargentina huyo ni;

1. Beno Kakolanya - Singida Fountain Gate

2. Yusuph Kagoma - Singida Fountain Gate

3. Frank Carlos Zouzou - Asec Mimosas

4. Serge Pokou - Asec Mimosas

5. Khanyisa Mayo- Cape Town.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo inaeleza juwa, mpaka sasa klabu ya Yanga itawaongezea wachezaji hawa wanaomaliza mikataba yao ambao ni;

1. Djigui Diarra

2. Bakari Mwamnyeto

3. Clement Mzize.

4. Aziz Ki.

Aidha, wachezaji wengine wataboreshewa mikataba yao kutokana na kiwango nzuri walichokionyesha.

Yanga imepanga kumaliza usajili mapema ili kuruhusu utambulisho ufanyike mapema kabla ya ligi kuu kuanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live