Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi amtaka Kagoma, Injinia Hersi aingia chimbo

Yusph Kagoma Gamondi amtaka Kagoma, Injinia Hersi aingia chimbo

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imeanza harakati za kunasa saini ya kiungo mkabaji wa Klabu ya Singida Fountain Gate, Yusuph Kagoma kwa ajili ya kuimarisha safu yao ya kiungo msimu ujao.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa, Kocha Miguel Gamondi amekuwa akimfuatilia Kagoma katika mechi nyingi na amevutiwa na uwezo wa kiungo huyo na anataka ajumuishwe kwenye kikosi chake msimu ujao.

Tayari Injinia Hersi ameshaanza mazungumzo na mchezaji huyo kuona uwezekano wa kumchukua kama mbadala wa Zawadi mauya ambaye mkataba wake unamalizika na hayupo kwenye mipango ya timu hiyo msimu ujao.

Yanga imepanga kumsajili Kagoma kwa usajili wa ndani huku jicho lao kubwa likiwa kwa mshambuliaji aliyeachana na Azam FC hivi karibuni, Prince Dube raia wa Zimbabwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: