Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi amsikilizia Pacome Sauzi

Aziz Ki Pacome Okrah A0003 Gamondi amsikilizia Pacome Sauzi

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa timu yake imekwenda Afrika Kusini kwa lengo moja tu la kutafuta ushindi na kufuzu kwenda nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na si vinginevyo.

Gamondi amesema hayo leo Alhamisi Machi 4, 2024 wakati akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa kesho nchini humo.

"Ni kweli Pacome Zouzoua amerejea kikosini na yupo fiti. Nina matarajio makubwa ya kufanya mabadiliko ya kikosi katika mchezo wetu wa marudiano. Wachezaji wanatakiwa kumwaga jasho ili kupata matokeo mazuri.

"Ukiwa na timu nzuri huwezi kuhofia mpinzani, malengo yetu makubwa ni kushinda mataji yote na kufanya vizuri zaidi. Tunajua tunaenda kucheza na timu ya namna gani, licha ya kuzuia ila tunahitaji kushambulia.

"Tunasubiri kuona itakavyokuwa leo kwenye mazoezi ya mwisho, tunaweza kumpata mchezaji katika wale waliokuwa majeruhi.

"Ni kweli tunaiwaza nusu fainali ya CAF lakini tunajali pia na usalama wa afya za wachezaji wetu pia. Young Africans haichezi mashindano haya peke yake. Tumejiandaa vema kufikia malengo ya kufuzu nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika," amesema Gamondi.

Wachezaji majeruhi ni Pacome Zouzoua, Khalid Aucho, Kibwana Shomari na Yao Koaussi ambao wapo kambini Afrika Kusini wakiendelea na mazoezi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live