Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi ampa 'mchongo' Dube, Fifa yawashukia

Gamondi Chama Dube Abuya 91021 Gamondi ampa 'mchongo' Dube, Fifa yawashukia

Fri, 23 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, akisema mshambuliaji wake, Prince Dube, anahitaji kuongeza umakini kidogo mbele ya lango la wapinzani ili kuweza kufunga mabao mengi, Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), limeita klabu hiyo kuilipa Bechem United FC ya Ghana Dola 80,000 sawa na Sh. milioni 216.9 za Tanzania.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Yanga kushindwa kesi iliyofunguliwa na Klabu ya Bechem FIFA, hicho ikiwa ni gharama ya ada ya uhamisho ya mchezaji Augustine Okrah waliyemsajili Januari mwaka jana.

Kwa mujibu wa barua ya FIFA kwenda Yanga iliyosambaa jana katika mitandao ya kijamii, klabu hiyo inatakiwa kuwalipa Waghana hao ndani ya siku 45 baada ya hukumu hiyo iliyotolewa jana.

Jitihada za kuwapata viongozi wa Yanga kuzungumzia maamuzi hayo ya FIFA hazikufanikiwa kwa kuwa simu za mkononi za viongozi hao ziliita bila majibu.

Kuhusu Gamondi na Dude, kocha huyo amesema ni mshambuliaji mzuri na mwenye uwezo mkubwa, lakini kuna baadhi ya mambo yanamfanya ashindwe kufunga mabao mengi.

Alisema tayari amekaa naye na kumpa maelekezo na kama atayafuata atakuwa miongoni mwa washambuliaji watakaokuwa wakifunga mabao mara kwa mara.

"Nataka muda mwingi tukiwa tunashambulia awe ndani ya eneo la hatari la wapinzani, tunatengeneza nafasi nyingi, lakini mara nyingi anakuwa hayupo eneo husika,

"Naamini akifanya hivyo na kuongeza umakini atakuwa akitufungia magoli mengi, ni mshambuliaji mzuri, ana nguvu na ufundi mwingi," alisema Gamondi.

Aidha, alisema kwa sasa anaendelea kuwapa maelekezo wachezaji wake kuelekea kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali dhidi ya Vital'O.

Kuhusu mchezo huo, Gamondi, alisema licha ya ushindi mnono walioupata kwenye mchezo wa kwanza wa mabao 4-0 katika Uwanja wa Azam Complex, hawatawadharau wapinzani wao hao.

"Bado hatujamaliza, tunamchezo wa pili nao ni muhimu, nataka kuona tunacheza vizuri zaidi na kupata ushindi mkubwa, tunaweza kufanya hivyo," alisema Gamondi.

Yanga itaumana na Vital'O Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kumalizia kazi waliyoianza wiki iliyopita ya kusaka tiketi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: