Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi amfunika Nabi Yanga

NABI GAMONDI MS Gamondi amfunika Nabi Yanga

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya jana Young Africans SC kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC, timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi imeweka rekodi mpya.

Young Africans SC ambayo jana imeibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons, imemaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC kwa kuendelea kukaa kileleni baada ya kucheza mechi 15.

Msimu uliopita kipindi kama hiki, timu ya Yanga baada ya kucheza mechi 15, pia ilikuwa kileleni, lakini kuna mabadiliko makubwa yamefanyika.

Katika mechi 15 za mzunguko wa kwanza msimu huu, Young Africans SC chini ya Gamondi, imekusanya pointi 40, kutokana na kushinda mechi 13, sare 1 na kupoteza 1.

Ukiachana na hilo, timu imefunga magoli 36, imeruhusu magoli 8, tofauti ya magoli ni 26, huku clean sheet zikiwa 9.

Rekodi za mzunguko wa kwanza msimu uliopita 2022/23, Young Africans SC chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, timu ilicheza mechi 15, ilishinda 12, ilipoteza 1 na sare 2.

Katika mechi hizo 15, timu ilikusanya pointi 38, yalifungwa magoli 27 na kuruhusu magoli 8, tofauti ya magoli ikiwa 19, wakati clean sheet zikiwa 9.

Ukiangalia rekodi za msimu uliopita 2022/23 chini ya Nabi na msimu huu 2023/24 timu ikiwa inanolewa na Gamondi, tofauti iliyopo ni katika idadi ya pointi, magoli ya kufunga, mechi tulizoshinda na sare. Lakini upande wa nafasi, clean sheet na mechi za kupoteza mambo yapo sawa.

Hiyo inaonesha kwamba, msimu huu kuna mabadiliko makubwa, hivyo mbio za kutetea ubingwa wetu wa ligi hiyo zinaonekana zipo katika njia sahihi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live