Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi amestahili kuwa kocha Bora wa Mwezi

Gamondi Tuzooo.jpeg Gamondi alistahili kuwa kocha Bora wa Mwezi

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa Radio, Samwel Rashid maarufu kama Wakanda Republic amesema kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amestahili kushinda Tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu ya NBC.

Wakanda amesema hayo baada ya Kocha huyo kushinda tuzo hiyo jana na kuwabwaga Kocha wa Simba, Riobertinho na yule wa Azam, Yousuf Dabo licha ya timu zao zote kushinda michezo yote miwili na kuwa na alama sita lakini Yanga ikiongoza kwa idadi kubwa ya mabao 10 ya kufunga bila kufungwa.

"Gamondi amestahili kuwa kocha bora wa mwezi kwa sababu timu yake ndiyo imeongoza kwa magoli, timu yake ndiyo imeongoza kwa performance nzuri.

"Timu yake ndiyo ambayo imeokota pointi nyingi kwenye hizi mechi mbili pointi 6 na hizo goli 10 kwenye mechi mbili, kwahiyo unaona kwenye kinyang'anyiro hichi dhidi ya walimu alioingia nao unaona kuna gape ambalo amewaacha," amesema Wakanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live