Azam FC imeshinda mechi 2 katı ya 3 na kutoka sare 1 ikikusanya alama 7 katı ya 9, hivyo kocha wake Bruno Ferry amemshinda Miguel Gamondi.
Azam iliifunga Yanga 2-1, ikaichapa Dodoma Jiji 4-1 na kutoka sare 1-1 na Coastal Union, hali iliyoibakisha kwenye nafasi yake ya pili kwenye msimamo.
Yanga SC wameshikilia nafanya yao ya kwanza kwa mwezi Machi na Azam FC wameshikilia nafasi yao ya pili kwa mwezi Machi.
Yanga ndiyo timu iliyofanya vizuri kwa mwezi Machi kuliko timu yoyote na Azam ndiyo timu ya pili kufanya vizuri baada ya Yanga, inakuaje kocha wa timu iliyofanya vizuri kupita nyingine anashindwa na yule anaemfuatia?
Ishu ya kocha bora ni performance ya timu, timu ipi imefanya vizuri kuliko Yanga mwezi Machi? Je ni kwakuwa Azam iliifunga Yanga ndipo Bruno amepitiamo? Kwahiyo mechi ya Azam na Yanga ndiyo ilikuwa maamuzi ya kocha bora na sio mechi za mwezi mzima?
Sidhani kama kamati ilijielekeza vyema katika eneo la kocha bora kwa maoni yangu.
Yanga imekusanya alama nyingi kuliko timuyoyote (9),imefunga mabao mengi kuliko nyingine (10) imeendelea kushika usukano wa ligi, performance ya timu ni ubora unaoanzia kwa kocha, kwanini sio Miguel Gamondi ni Bruno Ferry? Majibu wanayo wana Kamati ya tuzo za TFF
Jemedari Said