Mchambuzi wa soka Bongo Hans Rafael amesema, Kocha wa Yanga SC, Miguel Gamondi, ni kama amewaingiza chaka wapinzani wao Mamelodi kuelekea mchezo wao utakaopigwa mwishoni mwa mwezi huu Marchi.
Hans amesema ukiitazama mechi ya jana ya Yanga dhidi ya Geita, mfumo wa uchezaji wa Yanga ulibadilika.
"Set up ya timu ilibadilika jana kaanza na 4-3-3 Job alicheza kama namba 6 ambaye alikuwa anatengeneza back 3 ya uongo huku Aziz na Max wakiwa kama namba 8 lakini Augustine Okrah akiwa kama free role, dakika ya 23 Gamondi aliamua kuswitch Musonda kulia na Okrah kushoto, Max namba 8 na Aziz namba 10.
"4-3-3 iliwapa faida Yanga lakini ukweli ni kuwa fluidity hatukuweza kuiona, Yanga hawakuwa na rotation jambo ambalo linaonyesha Gamondi hakutaka Mamelodi Sundowns wasiweze kuona ubora wao na silaha zao," alisema Hans.