Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi amefungua nati ngumu yenye kutu

Yanga Gamondi Dodoma.jpeg Kocha Gamondi

Sat, 25 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwalimu anafika kurithi mikoba ya mwalimu aliyeipa ubingwa wa ligi klabu mara mbili mfululizo na katoka kucheza fainali ya kombe la shirikisho.

Mwalimu anarithi mikoba ya kocha ambaye kila mtu aliamini ni ngumu kupata mbadala wake ndani ya muda mfupi.

Mwalimu Gamondi anaichukua timu iliyotoka kumpoteza striker wake kinara aliyemaliza mfungaji bora kwenye ligi ya ndani na kombe la shirikisho. Analetewa striker ambaye anashindwa kuendana na kasi ya klabu lakini mwalimu hapati taabu.

Mwalimu aliweza kuyagawanya mabao kwa viungo wake wa juu. Akawapa mabao hawa kina Aziz K, Max Nzengeli, Mudathir Yahya na Pacome Zouzoua. Namna walivyokuwa wana”operate” kiwanjani ni ishara ya kazi kubwa ya mwalimu nyuma ya pazia.

Klabu imetetea taji lake la ligi, inakaribia kutetea taji la FA na imefika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa.

Mwanzo haukuwa mgumu kabisa kwa kocha Gamondi. Ni muendelezo wa mazuri ya Nasredine Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live