Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi amchimba mkwara Nabi Sauzi

Nabiii 0028 Nabi na Gamondi

Sat, 27 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Young Africans SC, Miguel Gamondi amesema uamuzi wa timu hiyo kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya pre-season ni sehemu ya kuendelea kuitangaza klabu.

Gamondi ameyasema hayo jana Julai 26, 2024 wakati timu yake ikiwa bado ipo Afrika Kusini huku ikitarajiwa kucheza dhidi ya Kaizer Chifes inayonolewa na aliyewahi kuwa kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi, kesho Jumapili Julai 28, 2024 katika Toyota Cup.

“Young Africans SC ujio wetu hapa Afrika Kusini umekuwa muhimu sana kwetu kwenye maandalizi kuelekea msimu mpya wa 2024/25 na kucheza na timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) ni sehemu ya kuendelea kuitangaza Klabu yetu barani Afrika na Duniani kote.

“Mchezo wetu dhidi ya Kaizer Chiefs utakuwa mchezo mzuri na wenye ushindani hasa ukizingatia Chiefs wana mwalimu mpya na kila mchezaji atapata nafasi ya kumuonesha mwalimu uwezo wake na kwetu sisi pia maandalizi yetu yanazidi kuimarika na tunaamini tutakwenda kuwa na mechi nzuri,” Kocha Mkuu Miguel Gamondi

Mpaka sasa Young Africans ikiwa Afrika Kusini, imecheza mechi mbili za Mpumalanga Cup dhidi ya FC Augsburg inayoshiriki Ligi Kuu Ujerumani ‘Bundesliga ambapo walipoteza kwa magoli 2-1, kisha wakaifunga TS Galaxy goli 1-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live