Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi alia na waamuzi, viwanja "Lakini hatuogopi"

Fd Nzengeli Gamondi Gamondi alia na waamuzi, viwanja

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amekiri kwamba ana wasiwasi na viwanja vya mikoani na vimechangia timu yake kutocheza vyema na kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Ihefu huku akiwatahadharisha waamuzi kutovumilia wachezaji wanaopoteza muda na kuharibu ladha ya mchezo.

Gamondi ametoa kauli hiyo leo Oktoba 6, 2023 jijini Mwanza wakati akizungumzia maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Geita Gold utakaopigwa kuanzia saa 10 jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Amesema siyo kwamba analalamikia maamuzi ya waamuzi kuiumiza timu yake bali anataka wazilinde timu zinazotaka kucheza mpira na siyo kuchekelea na kulea baadhi ya wachezaji na timu zinazoharibu ladha ya soka kwa matukio yasiyo ya kufurahisha uwanjani.

Aidha, amebainisha mchezo uliopita ulikosa ladha mbele ya mashabiki baada ya wachezaji wa Ihefu kujilaza chini bila sababu zozote na kupoteza muda huku wamauzi wakishindwa kuchukua hatua madhubuti.

"Kiukweli nina hofu na uwanja hatujafika kuuona lakini tutakwenda baadaye jioni, pia maamuzi ya waamuzi kwani baadhi ya timu zinapoteza muda na kuharibu kabisa ladha ya mchezo, nina imani kutakuwa na mabadiliko kwenye hili kwasababu kila kitu kinaonekana wazi," amesema kocha huyo na kuongeza;

"Nafahamu kesho tutakuwa na mchezo mgumu na sijui hali ya Uwanja ikoje lakini nafikiri itakuwa kama Uwanja wa mchezo wetu uliopita ambapo tulishindwa kucheza tulivyozoea kucheza pale Taifa na Chamazi

"Kwa hiyo nina wasiwasi na uwanja lakini hatuogopi, japokuwa hatutakuwa na possession tuliyoizoea na wachezaji watahitaji kufikiria sana ili kuendana na uwanja na kucheza vizuri."

Silalaimiki lakini waamuzi wanahitaji kuulinda mpira, watu wafurahie, tulinde timu inayohitaji kucheza mpira na siyo kupoteza muda," amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: