Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi alia na Ratiba akijiandaa kuwavaa Ihefu

Ngushi Gamondi Gamondi alia na Ratiba akijiandaa kuwavaa Ihefu

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga ikijiandaa kuivaa Ihefu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Oktoba 4 Jijini Mbeya.

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa ufinfu wa ratiba kwa upande wao imekuwa changamoto kubwa katika maandalizi ya kujiandaa na mchezo huo.

Akizungumza katika mkutano na waandisi wa Habari Gamondi amesema;

"Tunashukuru tumefika salama Mbeya, hatukuweza kupata muda mzuri wa kujiandaa kama mnavyojua tumetoka kucheza mchezo wa Kimataifa Jumamosi lakini tunajua umuhimu wa mchezo wa kesho dhidi ya Ihefu na tutafanya kila jitihada kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwenye mchezo huu"

Yanga mpaka sasa imecheza michezo mitatu ya Ligi Kuu na kushinda yote huku wakiwa ndio vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: