Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi alia na Dube, Aziz Ki

Gamondi X Dube Vita Gamondi na Dube

Fri, 30 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, analia na matumizi ya nafasi wanazotengeneza hasa kipindi cha kwanza katika michezo yao ya hivi karibuni.

Amesema tatizo kubwa ambalo lilikuwa kwenye mchezo wao wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar ni kushindwa kutumia nafasi ambazo walizipata ndani ya uwanja.

Alhamisi, Agosti 29, Yanga ilikuwa Uwanja wa Kaitaba, Kagera Sugar 0-2 mabao yalifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 25, Clement Mzize dakika ya 88 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Gamondi amesema wamekuwa shida ya kutumia nafasi ndani ya kipindi cha kwanza, kilichokoea wanarudi uwanja wa mazoezi kukifanyia kazi ili kuwa imara kwenye mechi zinazofuata.

Akizungumza mchezo na Kagera Sugar, amesema umekuwa mchezo wenye ushindani mkubwa kipindi cha kwanza kwa kutengeneza nafasi zaidi ya sita na kupata bao moja.

“Kipindi cha pili tulipata nafasi tatu tukatumia moja, sio mbaya kwa hili lililotokea kikubwa ni pointi tatu na makosa yaliyotokea tunakwenda kufanyia kazi eneo la mazoezi,” amesema Kocha Gamondi.

Ameongeza kuwa kilichotokea wanaenda kufanyia kazi kujiandaa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CBE SA ya Ethiopia , utakuwa mgumu kwao.

“Ukizingatia wachezaji ambao watakuwa kwenye timu ya taifa na watarejea muda mfupi, kuna kazi kubwa tunakwenda kufanya ninaimani tutafanya maandalizi mazuri kwa muda ambao tutaupata kujiandaa dhidi ya CBE SA,” amesema kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live