Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi alia na Aziz Ki "Guede bado sana!"

Cb Guede Aziz Ki Gamondi alia na Aziz Ki "Guede bado sana!"

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa, amefunguka alichowaambia wachezaji wake wakati wa mapumziko kwenye mchezo wa jana dhidi ya Mashujaa FC baada ya wachezaji hao kuumia wakati mchezo ukiendelea.

Gamondi amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari baada ya kumalizika kwa mchezo huo huku Yanga ikionekana kusua sua kupata matokeo katika michezo yake mitatu iliyocheza ikitoa sare moja na kushinda miwili, ikifunga mabao matatu na kufungwa bao 1.

"Ni kweli hatupati ushindi kama walivyozoea mashabiki wetu, ni jambo la kawaida kwenye soka, tumerudi kwenye ligi hatukuwa vizuri sana, kuanzia mchezo wa kwanza (dhidi ya kagera), lakini kwa sasa tunaendelea kuimarika.

"Tumemkosa mchezaji mhimu Aziz Ki kwenye mechi hizi, Joseph Guede naye bado mgeni ndiyo kwanza anaingia kwenye timu, Musonda naye ndiyo amerejea, wakati mwingine lazima tuwe wavumilivu. Jambo la mhimu tumeweka mpira kwenye nyavu," amesema Kocha Gamondi.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC, uliopigwa katika Dimba la Azam Complex, Chamazi, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 2-1, dakika za lala salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live