Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi aipigia hesabu Simba

Gamondi Kambini Yanga Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi.

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema ushindi wa mabao 2-2 waliopata katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Fountain Gate FC umewaongezea morali wachezaji wake kuelekea mchezo ujao dhidi ya Wekundu wa Msimbazi.

Watani wa jadi, Simba na Yanga wanatarajia kukutana katika mechi ya mzunguko wa kwanza itakayochezwa Novemba 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Gamondi aliliambia gazeti hili jana anawapongeza wachezaji wake kwa kupambana na kupata matokeo chanya dhidi ya Singida Fountain Gate na sasa wanatumia mapungufu ya mchezo huo ili kujiimarisha kuelekea mechi ijayo ya dabi.

Kocha huyo alisema ushindi huo ni mwanzo na unawapa nguvu ya kuendelea kujenga kikosi imara kwa ajili ya kusaka matokeo bora dhidi ya Simba.

"Tumefanikiwa kupata alama tatu katika mchezo wa leo (juzi), haukuwa mchezo rahisi, tumecheza vizuri lakini nimeona changamoto na nakwenda kuzifanyia kazi kujiandaa na mchezo ujao.

Mwisho wa mchezo huu ni maandalizi ya mchezo wetu ujao, tunafanya maandalizi kulingana na mpinzani tunayeenda kukutana naye, kwa sasa tunajiandaa kucheza na Simba, ni dabi, tunatakiwa kuwa makini ili kutetea taji hili kwa kufanya vizuri,” alisema Gamondi.

Kocha huyo alisema ni mapema kuanza kuzungumzia mchezo watakaocheza lakini sasa mipango yake ni kusahihisha makosa na kujiimarisha ili kutimiza malengo ya kushinda mechi hiyo.

Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate, Ricardo Fereira alisema walihitaji nguvu ya ziada katika mchezo ili wapate ushindi kwa sababu walifanya maandalizi mazuri lakini walishindwa kuondoka na pointi tatu.

Fereira alisema anajua ukubwa wa Yanga, unapocheza na timu kubwa unapofanya kosa unaadhibiwa lakini pia wachezaji wake walikuwa na presha.

"Nimeona baadhi ya maeneo ambayo nitayafanyia maboresho ya kiufundi, dakika ya 20 hadi 25 tulicheza vizuri na kutengeneza nafasi kadhaa, baada ya kufungwa bao akili yetu ikabadilika tukaanza kucheza kwa presha, ingawa tumepoteza lakini nimeridhishwa na kiwango cha wachezaji wangu,” alisema kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: