Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi aifunga busta, Skudu jukwaani Kirumba

Diarra X Skudu Gamondi aifunga busta, Skudu jukwaani Kirumba

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ameshtuka baada ya kipigo cha Ihefu, leo amejivua lawama mbele ya Geita Gold kwa kupanga kikosi kamili kilichoelezeka ili kuzisaka pointi tatu kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara inayopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, jijini hapa.

Yanga na Geita zinashuka uwanjani jioni, huku kila timu ikiugulia maumivu ya kipigo, Yanga ikifungwa na 2-1 Ihefu wakati Geita ikicharazwa pia 2-1 ikiwa nyumbani mjini Geita na KMC. a.

Katika kikosi kilichoanza leo, Gamondi raia wa Argentina amepangua na kuwapumzisha wachezaji saba walioanza kwenye kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Ihefu.

Kiungo wa Yanga aliyejizolea umaarufu, Skudu Makudubela ambaye mchezo uliopita hakuonyesha kiwango kizuri baada ya kucheza dakika chache leo amepumzishwa na yuko jukwaani akiwatazama wenzake wakimenyana na Geita Gold.

Nyota ambao wamepumzishwa leo ni mabeki Nickson Kibabage, Shomari Kibwana na Ibrahim Bacca, viungo Zawadi Mauya, Abubakar Salum 'Sureboy' na Skudu Makudubela pamoja na winga, Jesus Moloko.

Nafasi za mastaa hao zimechukuliwa na Kouassi Yao, Joyce Lomalisa, Dickson Job, Khalid Aucho, Maxi Nzingeli, Mudathir Yahya na Stephane Aziz Ki.

Kikosi cha Yanga: Diarra, Yao, Lomalisa, Job, Mwamnyeto, Aucho, Max, Mudathir, Mzize, Aziz Ki na ZouZoua.

Wachezaji wa akiba ni Abdultwalib Mshery, Nickson Kibabage, Gift Fredy, Gift Mauya, Sureboy, Denis Nkane, Jesus Moloko, Kennedy Musonda na Hafidh Konkoni

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: