Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi afyeka wawili wa Kimataifa

Moloko X Konkoni Gamondi afyeka wa Kimataifa wawili

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga Jesus Moloko rasmi amepewa barua ya kusitishiwa mkataba na Yanga baada ya kudumu klabuni hapo kwa miaka miwili na nusu.

Moloko amepewa barua leo Januari 15 asubuhi ya kuachwa na Yanga baada ya ripoti ya kocha wa timu hiyo Miguel Gamondi kuonyesha hayupo kwenye mipango yake.

Winga huyo Mkongomani nafasi yake inakwenda kuchukuliwa na Mghana Augustine Okrah ambaye tayari ameshapewa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwingine.

Mbali na Moloko Yanga pia inaachana na mshambuliaji Hafiz Konkoni ambaye amedumu klabuni hapo kwa miezi sita pekee.

Konkoni tayari ameshapewa barua ya kuachana na Yanga akirejea kwao Ghana baada ya kushindwa kuanza kwa kasi ndani ya timu hiyo.

Gamondi hakukubaliana na ubora wa mshambuliaji huyo na kuwataka viongozi kuachana naye kisha atafutiwe mshambuliaji mwenye makali zaidi.

Mwanaspoti linafahamu kuwa tayari mshambuliaji huyo ameshakabidhi nyumba aliyokuwa anaitumia ambayo Sasa itatumiwa na ndugu yake wa Taifa Moja Okrah.

Kuondoka kwa Konkoni Yanga inahaha kusaka mshambuliaji wa kuziba nafasi yake mchakato ambao unaendelea kuwakimbiza mabosi wa Yanga kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili leo saa 6:00 usiku

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: