Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi afunguka unyama wa Chama, Pacome na Aziz KI Kambini

Aziz Chama Pacome Yanga Gamondi afunguka unyama wa Chama, Pacome na Aziz KI Kambini

Sat, 13 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huko mtandaoni mambo yamekuwa mengi. Mjadala umekuwa ni namna eneo la mbele la Yanga linavyoweza kumpa ugumu kocha Miguel Gamondi kuamua aanze nani uwanjani na wachezji gani waanzie benchi.

Ndio wenye timu yao wamekuwa wakijadili zaidi kuanzia namba saba hadi 11, wakisema kwa namba hadi sita ni kama zina wenyewe, kwani wanamini Diarra Djigui, Yao Kouassi, Chadrack Boka, Ibrahim Bacca, Dickson Job na Khalid Aucho hakuna wa kuwagusa katika himaya zao.

Tatizo lilianzia kwa Yanga kumnasa Clatous Chama kutoka Simba, kisha juzi kati kati ijkamshusha Duke Abuya kutoka Singida Black Stars ambao ni viungo washambuliaji wanaoungana na Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya na Stephane Aziz KI.

Kisha ikamtambulisha tena Prince Dube aliyetokea Azam FC na jana ilimweka hadharani Jean Baleke aliyewahi kutamba na Simba ambaye amechukua nafasi ya Joseph Guede aliyekimbilia Singida Black Stars ambao wanaungana na Kennedy Musonda na Clement Mzize waliokuwapo kikosini tangu msimu uliopita.

Kuna wanaobeti kwamba huenda kati ya mastaa wa zamani na wapya, baadhi yao wataanzia nje ili kumpa kazi rahisi Kocha Gamondi, kisha mambo yakienda sivyo atatumia ule msemo wa toa sime lete bunduki, kwani kwenye benchi kutakuwa na watu haswa ambao watazidi kuifanya Yanga iwe tishio msimu ujao.

Hata hivyo kocha mkuu wa timu hiyo, ameweka wazi kwamba hana presha yoyote na wala hana mtihani mkubwa kama mashabiki wanavyodhani, ila akatoa salamu kwa wapinzani kwamba msimu huu watakuwa na kazi kubwa kukabiliana na timu hiyo inayoshikilia mataji ya Ligi na Kombe la Shirikisho.

Hata ukienda mazoezi ya Yanga utakutana na uso wa Gamondi ambaye huonekana kama anayefikiria kitu kadri anavyoona mastaa wa timu hiyo wanavyopasha, kisha ukaa na kufikiri kidogo na kuishia kutabasamu akiwaangalia wachezaji halafu,a naishia kuisema kwa mziki wa msimu ujao ninao.

Kauli hiyo ya Gamondi inatokana na aina ya usajili mpya ambao mabosi wa klabu walivyoufanya kwa kuingiza mashine mpya saba zenye uzito katika dirisha hili la usajili.

Kama hujui ni kwamba hadi sasa, Yanga imeshawasajili kipa Abubakar Khomeny, beki wa kushoto Chadrack Boka, viungo Aziz Adambwile, Clatous Chama, Duke Abuya wakati washambuliaji Jean Baleke na Prince Dube.

Usajili huo gumzo likawa eneo la kiungo ambalo ndio lilloipa mafanikio makubwa timu huyo kwa msimu uliopita likitoa pia mfungaji bora, Stephanie Aziz KI ambaye alikuwa akisaidiana na Maxi Nzengeli, Pacome Zouzua na Mudathir Yahya.

Viungo hao wanne tu ndio waliongoza kwa ufungaji ndani ya kikosi hicho ambapo Aziz akifunga mabao 21, Maxi (11), Mudathir (9) wakati Pacome alifunga saba na kufanya wote kufunga jumla ya mabao 48 kwenye mabao 71 ya kufunga.

Wakati msimu uliopita viungo hao wakiwa na balaa hilo la msimu uliopita msimu huu wakaongezwa Chama, Abuya na washambuliaji wengine wawili.

Wachezaji hao na wale waliokuwapo kikosini wote ni majembe na wanaongeza presha kubwa kwa mashabiki kutaka kujua nani atampisha nani katika kikosi cha kwanza, kwani wote ni vichwa kwelikweli.

MSIKIE GAMONDI

Hata hivyo, tofauti na presha za mashabiki, kwa Gamondi mambo ni tofauti kama alivyozungumza akiwasifu wachezaji wote wa kikosi hicho.

Akizungumzia usajili huo Gamondi alisema tofauti na wengine wanavyofikiri akisisitiza kwamba wala hana presha yoyote zaidi ya kufurahia aina ya kazi ambayo imefanywa na viongozi wake.

Gamondi ambaye msimu uliopita alichukua mataji mawili makubwa ya ndani, sambamba na kuifikisha Yanga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, alisema kwa sasa ana jeshi kamili litakalokuwa na uamuzi wake aanze na nani.

Kocha huyo raia wa Argentina alisema, presha itakuwa kwa wachezaji wenyewe kwani wanatakiwa kupambana kuanzia mazoezini hadi katika mechi ili afanye uamuzi wa kuanza na nani kisha nani atokee benchi.

"Ki ukweli najibu tena, sina presha kabisa yaani sina kabisa, kwangu nafurahia tu ujio wa wachezaji bora kama hawa tunategemea watajituma ili Yanga ifanikiwe, labda presha itakuwa kwao itategemea nani anajituma kuanzia mazoezini hadi kwenye mechi," alisema Gamondi na kuongeza;

"Unajua tupo hapa kuhakikisha tunafikia malengo yetu, tunataka kufika mbali zaidi kwenye mashindano makubwa ya Afrika, malengo kama haya lazima uwe na kikosi chenye hadhi kubwa kama hiki na kila mmoja wetu kujituma eneo lake.

"Nina furaha kwa kuwa tuna timu kubwa, viongozi wamefanya kazi kubwa kuwabakisha wachezaji tuliowataka na kupata wale bora wapya sasa tutaamua uanze na nani aanzie benchi, msimu uliopita kuna eneo tulipata shida, tunafahamu haitakuwa rahisi kila timu imejipanga lakini msimu ujao tutakuwa imara zaidi, tutapambana na yoyote.

Yanga inaendelea kujifua kenye kambi iliyopo Avic Town, Kigamboni jijini Dar es Salaam kabka ya kwenda Afrika Kusini kushiriki michuano maalumu ya Toyota Cup na Agosti 4 itatayumbulisha mziki mzima wa 2024-2025 katika Kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi kabla ya siku nne baadae kuvaana na Simba katika Dabi ya kwanza ya Ngao ya Jamii , ikirejea fainali ya msimu uliopita na kulala kwa penalti 3-1 jijini Tanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: