Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi afunguka safari ya ubingwa ilivyokuwa ngumu

Gamondi Hersi Gamondi afunguka safari ya ubingwa ilivyokuwa ngumu

Tue, 14 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Young Africans SC, Miguel Gamondi, amezungumzia safari nzima ya msimu huu hadi kufikia kubebwa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.

Ubingwa huo ni wa 30 kwa jumla na wa tatu mfululizo ambapo tumeubeba baada ya kuifunga Mtibwa Sugar magoli 3-1 wakifikisha pointi 71 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote katika mechi zilizosalia.

Katika safari hiyo ya ubingwa, Young Africans imecheza mechi 27, imeshinda 24, sare 2 na kupoteza 2. Magoli ya kufunga 60 yakiwa ni mengi zaidi, huku wakiruhusu kufungwa magoli 13 ambayo ni machache zaidi.

“Ninajisikia fahari, ni zaidi ya furaha kuwa katika familia hii, nadhani ubingwa huu wa 30 ni maalum, nina furaha kwa Wananchi wote.

“Wakati tunaanza ulikuwa ni msimu mgumu kwa sababu kila timu ilikuwa ikijiandaa kuja kuifunga Yanga.

“Lakini mbali na hayo yote umekuwa msimu mzuri sio kwamba ya mafanikio haya bali kwangu furaha kubwa ni kuona aina ya soka tulilokuwa tukicheza na kuwa mabingwa, ni kitu ambacho siwezi kukusahau katika maisha yangu,” alisema Gamondi.

Zimebaki mechi tatu za kumaliza msimu huu ndani ya Ligi Kuu ya NBC ambapo Yanga watacheza kukamilisha ratiba dhidi ya Dodoma Jiji (ugenini), Tabora United (nyumbani) na Tanzania Prisons (nyumbani).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live