Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi afunguka sababu ya kuwatoa Pacome na Aucho

Pacome Aucho Gamondiii (2) Gamondi afunguka sababu ya kuwatoa Pacome na Aucho

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa, alifanya maamuzi magumu ya kuwatoa nyota wake Khalid Aucho na Pacome Zouzoua kwenye mchezo wa jana dhidi ya Mashujaa FC baada ya wachezaji hao kuumia wakati mchezo ukiendelea.

Gamondi amesema hayo baada ya maswali kuwa wengi kutoa kwa mashabiki wakihoji kwa nini aliwatoa Pacome na Aucho na kuwaingiza Augustine Okrah na Jonas Mkude kisha muda mchache baadaye Mashujaa wakasawadhisha bao.

"Walionekana kuumia ikabidi niwapumzishe kuhofia michezo mingine mbeleni, tuna michezo migumu ugenini na dhidi ya CR Belouizdad, tunahitaji kuwa makini sana.

"Kama mchezaji anapopata majeraha na utaendelea kumuacha aendelee kucheza basi ukubwa wa jeraha hata kama lilikuwa dogo basi linaongezeka zaidi," amesema Kocha Gamondi.

Hata hivyo, katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC, uliopigwa katika Dimba la Azam Complex, Chamazi, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 2-1, dakika za lala salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live