Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga sc Miguel Gamondi akielezea sababu ya kufanya programu ya mazoezi ya leo ambayo yamefanyika katika ufukwe wa Coco Jijini Dar es salaam.
Leo ni Mazoezi ya kwanza kwa wachezaji wa Yanga mara baada ya kupewa siku mbili za mapumziko.
"Tuliwapa wachezaji mapumziko ya siku mbili kwa kuwa tulicheza mechi 4 ndani ya siku 10. Tumekuja hapa ufukweni kufanya mazoezi angalau Kubadilisha mazingira, kufanya mazoezi ya kuongeza kasi pamoja na nguvu.
"Nadhani pia ni nzuri kwa akili kwa kuwa inabadilisha mazingira na nina furaha kwa kuwa Kumekuwa na watu pembeni yetu wakitazama namna wachezaji wanavyofanya mazoezi kwa hiyo nina furaha sana.
"Mara zote huwa nasema ushindi unaanzia hapa mazoezini na kufanya kazi kwa bidii kunalipa," amesema Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga sc Miguel Gamondi.