Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi afunguka mazito kuelekea Fainali Mkwakwani Tanga

Gamondi X Robertinho Tanga Gamondi, Robertinho wafunguka mbinu zao kuelekea Fainali kesho

Sat, 12 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Yanga, Muargentina Miguel Angel Gamondi amesema kwamba mchezo wa Fainali ya Ngao ya Jamii kesho dhidi ya Simba SC utakuwa mgumu kwa sababu zinakutana timu bora.

Watani hao wa jadi wanakutana kesho katika Fainali ya Ngao ya Jamii Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga kuanzia Saa 1:00 usiku, mechi ambayo itatanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Azam FC na Singida Fountain Gate Saa 9:00 Alasiri.

"Utakuwa mchezo mkubwa na mzuri kwetu hasa kwa mwanzo wa msimu na najua umuhimu wa mchezo huu kwa kila mmoja wetu," amesema Miguel Angel Gamondi na kuongeza.

"Ni furaha kwangu kucheza mchezo huu mkubwa kesho, matarajio yetu ni kufanya vizuri na tumejiandaa bila presha yoyote, kwa sababu nimeshakutana na michezo ya aina hii mingi, tunaenda kupambana kwa ajili ya nembo ya Yanga na mashabiki wetu ambao wapo nasi kiła siku,".

Kwa upande wake beki, Dickson Job amesema; "Kwa upande wetu wachezaji tuko tayari na mchezo wa kesho na tumejiandaa vizuri tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kutupa nguvu uwanjani," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: