Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi afunguka ishu ya kuachwa Pacome, Diarra

Aucho, Pacome, Diarra, Lomalisa Kuikosa Namungo Leo Gamondi afunguka ishu ya kuachwa Pacome, Diarra

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya maswali mengi kuhusu kuachwa kwa mastaa sita wa kikosi cha kwanza cha Yanga, kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi ametoa sababu za kuachwa nyota hao.

Yanga iko katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 43 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kushinda mechi 14, sare moja na kipigo kimoja kwenye mechi 16 ilizocheza hadi sasa, msimamo ambao unaongozwa na Azam FC yenye alama 44.

Wachezaji walioachwa kwenye msafara wa Yanga ambayo inacheza na Namungo jioni ya leo ni Djigui Diarra, Joyce Lomalisa, Khalid Aucho, Keneddy Musonda, Pacome Zouzoua na Joseph Guede.

Gamondi amesema anatambua umuhimu wa wachezaji hao kikosini kutokana na mchango mkubwa walioutoa kwenye michezo iliyopita, lakini ameamua kuwapa muda wa kujitibia majeraha madogo madogo waliyoyapata na wengine kumaliza matatizo waliyonayo.

"Kwa asilimia kubwa ni wachezaji muhimu kikosini, lakini wana shida ambazo tungeziweka pembeni ingeleta shida kwani wasingecheza kwa ubora tunaoufahamu kutoka kwao," amesema.

"Sipendi kuweka wazi shida ya kila mmoja inatakiwa kueleweka kuwa kuna ambao wana majeraha madodomadogo na wengine shida za kifamilia."

Pia, Gamondi amesema itachangia kuwapa muda wa kuwa fiti zaidi kwa mechi nyingine zilizo mbele yao huku akiitaja Ihefu FC na Geita Gold michezo ambayo watacheza uwanja wa nyumbani.

"Baada ya mechi ya leo na Namungo tutakuwa na siku mbili tu tayari kwa mchezo mwingine wa ligi, hivyo kutoa nafasi za baadhi ya wachezaji ambao hawapo fiti kutokana na majeraha madogo madogo itatusaidia," amesema kocha huyo.

Chanzo: Mwanaspoti