Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi afumua mfumo Yanga, Maxi, Mudathir wapewa majukumu mapya

Zx Maxi Mudathir Gamondi afumua mfumo Yanga, Maxi, Mudathir wapewa majukumu mapya

Sat, 2 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Angel Miguel Gamondi amefanya mabadiliko makubwa aloyofanya ndani ya kikosi chake ikiwa ni pamoja na kuwabadilishia majukumu baadhi ya nyota wake.

Moja ni kubadilisha majukumu ya kinafasi kati ya viungi Maxi Mpiah Nzengeli na Mudathir Yahya Abbas.

Wakati anafunga bao dhidi ya CR Belouizdad, Mudathir alitoboa siri ya kufunga mara kwa mara akasema kocha wake huyo amembadilishia majukumu kama kiungo wa kati, na sasa anacheza kama false winger (mshambuliaji wa pembeni) lakini akiwa na uwezo wa kuingia ndani.

Katika mabadiliko hayo ya kimfumo, Mudathir kwa sasa amepewa jukumu la kufika zaidi kwenda kwenye 18 ya wapinzani huku Mazi akitakiwa kusalia zaidi kwenye nafasi yake katikati ya uwanja, na kuingia kwenye 18 ya mpinzani mara chache mno.

Hii ndio sababu Mudathir Yahya anafunga sana, na Maxi Nzengeli amesimama kwenye kufunga.

Gamondi amefanya hivyo baada ya kubaini Maxi ni mzuri kwenye kupasia kwa usahihi kuliko Mudathir. Na kwa namna Yanga wanavyofunguka mabao yao, wakiwa wanashambulia inatakiwa viungo wa kati kuwa na usahihi wa kupasia ili kutopoteza mipira wakapigwa shambulio la kujibu.

Mudathir ana nguvu ya kukimbia maeneo mengi kuliko Maxi. Hivyo kwake ku-cover eneo kubwa sio shida na pia ana mikimbio mizuri kwenda kwenye 18 ya wapinzani kama third man striker ambaye anatumika kuvuruka mipango ya adui na kufunga hasa akiwa nyuma ya mabeki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live