Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi afichua siri ya mavitu matamu Yanga

Gamondi Yanga Yake Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya mechi ya ‘Kariakoo Derby’ ataja mambo manne yanayoibeba tmu hiyo na yaliyowapa ushindi jana Kariakoo Dabi.

Gamondi ameandika “Siri? Ni kupambana, kupambana na kupambana pamoja na kipaji, nidhamu na furaha yakuwa kwenye timu hii”

Yanga jana imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhdi ya Simba katika Uwanja wa Mkapa yakifungwa na Kennedy Musonda kipindi cha kwanza, Maxi Nzengeli akifunga mawili kipinid cha pili, Aziz KI na msumari wa mwisho ulipigwa dakika ya 87 kupitia kwa Pacome Zouzoua aliyefunga kwa mkwaju wa penalt baada ya Che Malone kumfanyia madhambi Nzengeli katika eneo la hatari.

Yanga jana ilirudi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kwa kishindo ikiandika historia kwa kuwachapa watani wao wa jadi, Simba mabao 5-1, lakini yakiwa ni malipo ya mwaka 2012 ambao Simba iliwachapa Yanga mabao 5-0.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: