Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ametaja siri mbili ambazo zinaipa faida Yanga na kuanza vyema katika michezo yao yote ambayo wamecheza mpaka sasa katika msimu wake wa kwanza ndani ya timu huyo.
Gamond alifichua siri mbili juu ya ubora wa Yanga huku akigusia kuwa benchi lake la ufundi chini ya kocha msaidizi kutoka Senegal, Mousa Ndaw na kocha wa viungo wa timu hiyo ni sehemu ya mafanikio ya timu hiyo kwa kuwa wamekuwa na utashi mkubwa sana na mbinu nyingi za kuifanya timu kuwa bora.
Kocha huyo pia aliongezea siri nyingine ya pili kuwa uwezo wa wachezji wake wengi kuwa na uwezo wa kufunga mabao ni silaha kubwa ambayo anayo jambo ambalo limepelekea kuwa na uhakika wa kupata bao katika kila mchezo ambao watacheza.
“Cha kwanza siri kubwa ya mafanikio ya Yanga ni kutokana na uwepo wa benchi langu la ufundi chini ya kocha msaidizi Ndaw,kocha wa Viungo na daktari wa timu na wengine wote kama meneja,hawa wamekuwa na uwezo mkubwa sana katika kutambua vitu na kufahamu nini cha kufanya.
“Watu wanaweza waka wanaona kuwa ni mimi pekee ndiye nnayefanya kazi hii kubwa kiasi cha Yanga kufanikiwa lakini kuna watu makini,ndani ya Uwanja nafurahia kuwa na timu ambayo inawachezaji wengi wenye uwezo wa kufunga mabao nah ii faida kubwa sana kwetu,inatupa uhakika wa kila mechi kupata mabao.
“Nafurahia kwa kuwa tunakuwa hatumtegemei mchezaji mmoja pekee kufunga mabao na badala yake tunakuwa tunaimani na timu nzima,nah ii ndio timu ambayo kila mtu angetamani kuwa nayo,tunaendelea kujiboresha zaidi kwa kuwa safari bado ni ndefu,” alisema kocha huyo