Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi aficha faili la CAF

Yanga Gamondi Wachezaji Gamondi aficha faili la CAF

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amekiri timu hiyo ipo katika kundi gumu la michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika linalohusisha mabingwa halisi pekee, lakini amesema kwa sasa hataki kuanza kuwafikiria zaidi wapinzani hao na badala yake kuelekeza nguvu zaidi kwenye mechi za Ligi Kuu watakazocheza awali.

Yanga imepangwa Kundi D na timu za CR Belouizdad ya Algeria, Medeama ya Ghana na Al Ahly ya Misri ambao wote ni mabingwa wa msimu uliopita wa ligi za nchi zao kama ilivyo kwa vijana wa Jangwani waliotetea taji kwa msimu wa pili mfululizo.

Akizungumza nasi, Gamondi alisema kwa sasa hataki kuchanganya mambo kwa vile akili ya kikosi hicho kinatakiwa kuangalia mechi za hivi karibuni za Ligi Kuu Bara kabla ya kuanza kampeni yao ya mechi za makundi za ligi hiyo ya CAf inayoanza hatua hiyo kuanzia Novemba 25.

Yanga itakuwa na mechi nne za ligi kabla ya kuanza mechi za makundi ratiba ikionyesha watakutana Azam Oktoba 25, kisha kuikaribisha Singida Big Stars, Oktoba 28 halafu itacheza na Simba ikiwa wageni Novemba 5 na baadae kuifuata Coastal Union, jijini Tanga wiki moja baadae.

Yanga itaanzia ugenini mechi za makundi akiwa wenyeji wa CR Belouizdad ya Algeria mechi itakayopigwa kati ya Novemba 24-25, kabla ya kurudi nyumbani kukutana na watetezi Al Ahly ya Misri mechi ikipigwa kati ya Desemba 1-2.

Gamondi alisema akili yake kwa sasa inataka kuangalia mechi nne za ndani ambazo ndizo zinazoweza kuwaongezea ubora kabla ya kuanza kampeni yao ya makundi.

“Tupo kundi gumu nafikiri mtaona ni kama mabingwa halisi wa kila nchi wamekutana kundi D, kuna kazi ambayo tunatakiwa kuifanya lakini kwa sasa sitaki kuangalia hizo mechi, tuna ratiba ngumu ya ligi ya ndani nafikiri hili linatakiwa kutangulia,” alisema Gamondi na kuongeza;

“Mechi za ndani zimekuwa na ugumu wake kwanza ushindani, pia ratiba yenyewe nayo inatutaka kuwa makini zaidi kutokana na mechi kukaa karibu karibu, tukikosea mechi hizi tutajiondoa kwenye utulivu wa hizo mechi za Ligi ya Mabingwa.”

Pia kocha huyo alisema kila timu zilizopo kundi hilo zinaendelea kujipanga, huku akionyesha jinsi gani zinakutana na wakati mgumu kwenye mashindano mengine.

“Tumetoka kupoteza mchezo wa ligi dhidi ya Ihefu lakini ukiangalia Belouizdad nao wamepoteza mechi ya ligi wakati sisi tukishinda, Ahly nao wamepoteza mechi ya Super cup ingawa sasa wanashinda, haya yote ni mazingira ya kujiimarisha, unapopoteza unaangalia wapi uboreshe,” alisema Gamondi aliyeiongoza Yanga kwenye mechi 11 za mashindano yote, ikishinda tisa na kupoteza mbili, ikiwamo ya Ngao ya Jamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: