Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi afanye haya kuwafunga Mamelodi

Yanga Vs Mamelodi Yanga wafanye haya kuwafunga Mamelodi

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa hesabu za haraka ni kwamba Yanga ina mlima mrefu wa kuupanda kutokana na rekodi tamu za Mamelodi kwa miaka ya hivi karibuni.

Hata hivyo, kwa aina ya kikosi ilichonacho Yanga kwa sasa chini ya kocha Miguel Gamondi na kama itacheza soka kama ililocheza dhidi ya CR Belouizdad nyumbani, kuna nafasi kubwa kwa vijana wa Jangwani kuishangaza Afrika.

Licha ya Mamelodi kuonekana tishio, lakini inafungika kwani katika mechi sita za makundi ilipoteza mechi moja ugenini dhidi ya TP Mazembe, na ilifunga jumla ya mabaao saba ikiwa na wastani wa kufunga bao moja tu kwa kila mechi, lakini tishio jingine kwa wababe hao ni kwamba hawaruhusu mabao.

Walifungwa bao moja tu katika mechi sita za hatua ya makundi, kitu ambacho Yanga ni lazima ijipange kwelikweli kuikabili timu hiyo. .

Yanga ni kati ya timu zilizomaliza na mabao mengi kwenye makundi ikifunga tisa sawa na Simba, lakini ni timu iliyoruhusu mabao sita yakiwa ni mengi miongoni mwa timu Nane Bora zilizotinga robo fainali kwa msimu huu .

Yanga inapaswa kusuka upya ukuta wa timu yake kabla ya kukabiliana na Mamalodi yenye washambuliaji tishio kama Peter Shalulile, Lucas Costa, Thembinkosi ‘Nyos’ Lorch na wengine ambao wanajua kufunga.

Ibrahim Bacca, Dickson Job, Bakar Mwamnyeto na mabeki wa pembeni, Joyce Lomalisa, Nickson Kibabage, Yao Kouassi na kipa Diarra Djigui ni lazima wahakikishe wanacheza kwa nidhamu na kuwaheshimu Mamelodi kama walivyofanya mbele ya Belouizdad au Al Alhy kwa mechi za nyumbani ili kupata matokeo mazuri mbele ya Wasauzi.

Kocha Gamondi aliyewahi kuinoa timu hiyo ya Afrika Kusini, ni wazi kwa sasa atakuwa anaisoma upya Mamelodi kuona anatumia mbinu zipi za kuidhibiti nyumbani na ugenini.

Kitu cha muhimu ni kulitengeneza jeshi lake kuhakikisha kila nafasi wanazotengeneza uwanjani wanazitumia ili kupata ushindi mnono na kwenda kukomaa ugenini, ambako kwa msimu huu imekuwa haina rekodi nzuri kulinganisha na msimu uliopita iliposhiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live