Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi aanza rekodi mpya Yanga

Gamondi X Yanga Somo Gamondi aanza rekodi mpya Yanga

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati makocha wengine wakikuna vichwa jinsi ya kuwatumia wachezaji, hali ni tofauti kwa Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi kwani licha ya kukabidhiwa kikosi msimu huu tayari asilimia 99 ya nyota wote 26 wamecheza michuano mbalimbali huku Dickson Job na Kouassi Yao wakifunika.

Yanga imecheza mechi tisa kwenye mashindano mbalimbali ikiwa ni pamoja na mchezo mmoja wa wiki ya Mwananchi ambao ulikuwa maalumu kwa ajili ya kutambulisha kikosi cha msimu huu.

Katika mechi tisa, timu hiyo imefunga mabao 23 ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara moja.

Ushindi wa Yanga katika mechi zote hizo umechangiwa na kikosi chote kutokana na kocha Gamondi kutoa nafasi kwa kila mchezaji, huku kipa Abuutwalib Mshery akiwa ni pekee aliyekosa nafasi ya kucheza kutokana na kutoka kuuguza majeraha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: