Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi aanza kuwaandalia dozi Azam FC

Gamondi Chama Aziz Pacome Gamondi awaandalia dozi Azam FC

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga SC amesema kuwa mechi dhidi ya Azam Fc ya fainali ya Ngao ya Jamii utakuwa mzuri na wa kufurahisha kwa sababu mpinzani wao pia ana timu nzuri.

Gamondi amesema hayo jana baada ya kuwafunga Simba kwa mara ya tatu mfululizo kipigo cha bao 1-0 kwenye nusu fainali ya Ngao ya Jamii, mchezo uliopigwa katika Dimba la Mkapa.

“Mchezo dhidi ya Azam utakuwa mzuri, tutafurahia soka zuri kwa sababu Azam ni timu nzuri na wanacheza vizuri sana, kwangu ni njia nzuri ya kuanza msimu, tumetoka kucheza dabi dhidi ya Simba, mechi ijayo dhidi ya Azam na usisahau tumecheza mechi kubwa Afrika Kusini.

“Kesho (leo) tutafanya mazoezi ya recovery, baadaye tutaanza kujiandaa na mchezo wa fainali. Sisi tunaendelea kuimarisha kikosi chetu ili tuwe na msimu bora na tufikie malengo ambayo tumejiwekea msimu ujao,” amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: