Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi aanika siri ya kuwafunga Simba mara tatu mfululizo

Gamondi Fadlu Mez Gamondi aanika siri ya kuwafunga Simba mara tatu mfululizo

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ubora wa kikosi chake na kujituma kwa wachezaji wake ndivyo viliamua mchezo wa jana dhidi ya Watani wao wa Jadi Simba Sc na kuwafanya Wananchi kuibuka na ushindi kwa mara nyingine tena.

Gamondi amesema hayo jana baada ya kuwafunga Simba kwa mara ya tatu mfululizo kipigo cha bao 1-0 kwenye nusu fainali ya Ngao ya Jamii, mchezo uliopigwa katika Dimba la Mkapa.

“Ni mindset ya winning mentality ambayo tumeiweka kwa wachezaji kwamba lazima tushinde. Tumecheza mchezo mzuri sana, tumepambana sana leo na kupata ushindi, tunafuraha na ushindi huu ni maalum kwa ajili ya Wananchi. Sio kazi nyepesi kushinda mechi tatu mfululizo dhidi ya Simba lakini tunatakiwa kuendelea kupambana.

“Simba wamecheza vizuri lakini hawakutenegeneza hata nafasi moja ambayo ni hatari kwetu, sisi tulitengeneza nafasi tatu za wazi kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili walikuja kwa ari kubwa lakini tulibaki kwenye mpango wetu, Aziz Ki alifunga bao halali lakini mwamuzi akasema ni offside, pia ilikuwa penati halali faulo aliyofanyiwa Aziz lakini refa alikataa.

“Kwenye dabi lazima tucheze hivyo, sio lazima tutumie nguvu kubwa kupambana laki cha msingi ni kupata ushindi na leo wachezaji wetu wamecheza vizuri sana.

“Tumeshakuwa familia na wachezaji, wanajua tunachokitaka, tumetenegeza hii mindset kwenye uwanja wa mazoezi. Kipaji pekee hakitoshi kupata ushindi wa mchezo, unahitaji team work, intelligent na leo tulikuwa bora kwenye maeneo muhimu, ni hicho tu.

“Sifa zote ninawapa wachezaji wangu kwa sababu wamepambana na walikuwa na njaa ya kupata ushindi na hiki ndicho kitu cha muhimu kwangu,” amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: