Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi aanika mfumo atakaoutumia kesho kuwamaliza Simba

Gamondi Yanga Pacome Aziz Maxi Skudu Gamondi aanika mfumo atakaoutumia kesho kuwamaliza Simba

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa falsafa yake anaamini kutumia viungo zaidi kwenye mechi zake kwani ndiyo eneo linaloamua mchezo uchezweje.

Gamondi amesema hayo wakati akizungumza leo na wanahabari kuelekea mchezo wa Derby ya Kariakoo dhidi ya watani zao Simba SC, utakaopigwa kesho Jumamosi, Aprili 20, 2023 katika Dimba l Mkapa.

“Falsafa yangu inaamini zaidi kwenye kumiliki eneo la Kiungo, ukishika Kiungo umeshika mchezo mzima, unaweza kusema najaza sana watu eneo la Kiungo lakini lazima ujue nawatumiaje Stephen Aziz Ki na Pacome Zouzoua,” amesema Gamondi.

Yanga wana viungo wengi wa kati wakiwemo Aziz Ki, Pacome Zouzoua, Khalid Aucho, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya, Jonas Mkude, Salum Abubakary Sureboy, Shekhan Ibrahim.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live