Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi aandika mbinu za ASAS kesho "Nimeshawasoma"

Miguel Gamondi Xx Dickson Job Kocha Gamondi.

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema mchezo wao wa marudiano wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASAS FC ya Djibout utakuwa mgumu hivyo wamejipanga kukabiliana nao ili kupata matokeo chanya.

Gamondi amesema malengo ya Yanga ni kushinda na kusonga mbele katika hatua inayofuata hivyo wanajua mpinzani wao atakuja kwa kushambulia zaidi yao lakini yeye na benchi lake la ufundi wamejiandaa na mbinu nzuri za kuwakabili ASAS kesho katika Dimba la Azam Complex, Chamazi.

Katika mchezo wa kwanza, yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-0 hivyo wanahitaji sare hata ya bila kufungana ili kufanikiwa kusonga mbele katika hatua inayofuata.

"Tulicheza mchezo wa kwanza tukashinda, lakini tunajua kuwa ni michezo miwili, kwa hiyo tu, meshacheza mchezo wa kwana hapa Chamazi, tulifanya vizuri lakini tulikosa nafasi nyingi sana, pengine tulistahili kushinda mabao mengi zaidi yay ale tuliyopata.

"Kesho utakuwa mchezo wa tofauti sana, ninaamini watakuja kwa ajili ya kushambulia zaidi yetu, tumejiandaa kwa hilo. Tutaona itakavyokuwa lakini tumedhamiria kushinda Kamba ambavyo siku zote Yanga inataka kufanya. Ninaamini utakuwa mchezo mzuri kwa mashabikiwa Yanga," amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live