Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi aandaa mfumo mpya Yanga

Gamondi Miguel Tizi Gamondi aandaa mfumo mpya Yanga

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Miguel Angel Gamondi, ameanza kutengeneza mfumo mpya wa uchezaji ili kuwafanya wachezaji wake waweze kufunga mabao mengi, hasa kwa timu ambazo zinatunia mfumo wa kukaa nyuma ya mpira, mwanzo mwisho.

Gamondi ameamua kuwafundisha vijana wake jinsi ya kujipanga na kuachia mashuti makali ya mbali huku akiwataka si lazima wafike hadi langoni.

Akizungumza visiwani Zanzibar, kocha huyo amesema hakufundisha mfumo huo kwa ajili ya mechi ya Robo Fainali dhidi ya APR, uliomalizika kwa kikosi chake kupoteza 3-1 jana Jumapili (Januari 07), bali hata mechi zingine zinazofuata za Ligi Kuu pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya kutolewa kwenye Kombe la Mapinduzi, tuna michuano mingine mingi, mazoezi haya ni kwa ajili ya maandalizi yote kwani huu ndiyo muda mzuri wa kujiandaa tukitoka hapa na kumalizika AFCON hakutokuwa na muda tena,” amesema kocha huyo.

Ofisa Habari wa Young Africans, Ali Kamwe, amesema katika aina mpya ya mazoezi ya Gamondi alikuwa anadili na viungo, mawinga na washambuliaji tu.

“Gamondi katika mfumo huu au staili hii mpya ya uchezaji hana kazi na mabeki, anadili na viungo, mawinga na washambuliaji tu, zinapigwa pasi, mashuti.

“Yamefungwa mabao mengi sana siku ya kwanza ya mfumo huu mazoezini, zaidi ya mabao 17, zinapigwa pasi, halafu anawekewa mtu nje ya 18, Shekhan amefunga mabao kama sita pekee yake kwa mashuti ya mbali, Maxi Nzengeli naye ametandika mabao ya kutosha, Skudu (Mahlatse Makudubela) naye kafunga, naona huko mbele tutakuwa na staili nyingi za kufunga mabao na si mpaka tuingie ndani ya eneo la hatari,” amesema Kamwe.

Young Africans inashika nafasi ya pili katika Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 30, lakini inakamata nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi D, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ikiwa na pointi tano sawa na kinara Al Ahly ya Misri ambayo ina kiporo cha mechi moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live