Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi aambiwe ukweli, anafeli!

Pacome Gamondi Maxi Gamondi na wachezaji wake.

Sat, 25 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Yanga ilikosa Heshima Kwa Mpinzani wake CR Belouizdad jinsi ambavyo iliamua kuuendea mchezo huu hali iliyopelekea kuruhusu magoli matatu kwa mtungi ugenini.

Hakukuwa na haja ya kufunguka katika mchezo wa ugenini Plan kubwa ambayo ingetumika ingekuwa ni counter attack na kuzuia.

Gamondi aambiwe ukweli kuwa hii ni michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika na sio Kombe la Shirikisho wala NBC Premier League.

Ukweli usemwe, huwezi kucheza na CR Belouizdad kama unaenda kucheza na Dodoma jiji. Yanga ilifeli kwenye game Plan ya ugenini.

Mchezo unaofata dhidi ya Al Ahly ni mgumu zaidi ya huu waliocheza na CR Belouizdad isipojipanga kisawasawa tutarajie ikienda kupoteza mchezo mwingine wa pili kama watacheza hivi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live